MWADUI itacheza na Simba keso alhamisi lakini Kocha wa zamani wa Toto Africans, Stand United, Muhibu Kanu amewaambia wachimba madini hao kama wanataka kuwamaliza Simba ni lazima wawakamate wachezaji watatu wa kikosi hicho.
Kanu alisema Simba ya sasa si ile ya mzunguko wa kwanza hivyo kama Mwadui wanataka kushinda mpambano huo ni muhimu kupambana vilivyo ndani ya dakika 90.
Alisema Mwadui wanatakiwa kuhakikisha Saidi Ndemla awezi kucheza kwani kwa sasa amekuwa msaada mkubwa kutoa pasi za mwisho ambazo zimekuwa zikiwapa Simba mabao.
“Ukiangalia Simba ya sasa Said Ndemla ndio anawapikia mabao kina Emmanuel Okwi na John Bocco sasa kama ukitaka kuwathibiti wekundu wa Msimbazi ni lazima Mwadui wahakikishe huyu kiungo achezi kabisa”alisema Kanu.
Hata hivyo alisema pia Mwadui wanatakiwa kuwa makini na Shiza Kichuya ambaye kwa mfumo wa 3-5-2 wanaotumia Simba kumfanya awe mpikaji mkubwa wa pasi za mwisho.
“Shiza Kichuya kwa sasa amekuwa msaada mkubwa kwa kutoa pasi za mwisho na wakati mwingine kufunga mabao hivyo wanatakiwa kumbana ili asiweze kucheza”alisema.
Alisema kama Mwadui wakifanya hivyo basi wataweza kuwamaliza Simba kwani wakiweza pia kuhakikisha wanalimiliki eneo la kati basi kina John Bocco na Emmanuel Okwi hawatoweza kufunga mabao.
No comments:
Post a Comment