Msanii wa muziki Bongo, Mbosso amesema mashabiki wanaomchukulia kwamba amekuja kwenye Bongo Flava ili kuleta ushindani kwa Aslay ni mitazamo yao tu.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Watakubali’ amesema anaheshimu kile anachofanya Aslay wala hajafikiria kuja kushindana naye.
“Mimi naheshimu muziki wa Aslay kwa sababu ni mtu ambaye nimemkuta kwenye Industry, halafu kwangu mimi yule ni brother, tunaheshimiana na muheshimu sana,” amesema Mbosso.
Mbosso ambaye hivi karibuni alijiunga rasmi na label ya WCB alikuwa ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wakiunda kundi la Yamoto Band kwa kushirikiana na Aslay, Beka na Enock Bella.
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment