Nyota wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva wa Difaa El Jadida, amewasiliasubuhi ya leo Alhamisi kwa mapumzikomafupi baadaya Ligi Kuu Morocco 'Batola Pro' kusimamakwa muda.
Msuva ameifungia Difaa mabao matano kwenye michezo 14 kati 15 ambayo ameichezea timu hiyo kwenye mzunguko wa kwanzawa Batola Pro ambao umemalizika.
"Nitakitumia kipindihiki chamapumzikomafupi kwa kuwakaribu nafamilia yangu, nitakuwa hapakwa wiki mojanabaada ya hapo nitarejeaMorocco," amesemamchezaji huyo wa zamani wa Yanga.
Hatahivyo Msuva amekiri kuendeleakuwepo kwa changamotoya mawasiliano kutokananawakazi wengi wa nchi hiyo kuzungumza Kiarabu naKifaransa.
"Haiwezi kuwa haraka hivyo, itanichukua muda kuanzakuzungumza vizuri lughazao japokwa sasa kunabaadhi ya maneno yao mepesinimejifunza," amesema.
No comments:
Post a Comment