TUNDU LISSU AFURAHISHWA NA UJIO WA BOMBARDIER Q400 AFUNGUKA HAYA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 31 March 2018

TUNDU LISSU AFURAHISHWA NA UJIO WA BOMBARDIER Q400 AFUNGUKA HAYA.

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA Mh. Tundu Lissu ambaye kwa sasa yupo kwenye matibabu nchini Ubelgiji ameonyesha kufurahishwa sana na ujio wa ndege aina ya Bombardier Q400.



Tundu Lissu baada ya kusema hayo amewataka wasemaji wa serikali waweke wazi ni sababu zipi zilipelekea ndege hiyo kushikiliwa nchini Canada na pia waweke wazi taarifa za kuachiliwa kwa ndege hiyo. 
"Msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa, na kabla yake Msemaji wa Serikali, Abbas, hawajasema, hadi sasa ni kwa nini Bombardier yetu ilikuwa imezuiliwa Canada. Hawajasema kama ni kweli au la kwamba ndege yetu ilikuwa imezuiliwa kwa sababu kuvunjwa mkataba kimakosa na aliyekuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wakati huo. Nafurahi kusikia taarifa za kuachiliwa kwa ndege yetu. Nitafurahi zaidi tukiambiwa Bombardier hiyo imeachiliwa kwa masharti gani, kwa vile tulikuwa tunadaiwa karibu USD milioni 40 zilizotokana na kuvunjwa mkataba na Serikali kushindwa kesi na SCEL. Hili ni swali ambalo kila mmoja wetu anatakiwa kuwahoji hawa watoa taarifa za kuachiliwa kwa Bombardier" alisema Tundu Lissu 
Baada ya jana taarifa kusambaa juu ya kuachiwa kwa ndege hiyo kuna watu walianza kudai kuwa ujio wa ndege hiyo ni pigo kwa watu ambao walikuwa sababu ya ndege hiyo kushikiliwa Canada, hivyo Tundu Lissu ametaka hao watu wafahamike kwa serikali kutoa sababu zilizopelekea ndege hiyo kushikiliwa Canada kabla ya kuachiwa jana. 
"baadhi ya watu wamedai mitandaoni kwamba kuletwa kwa ndege hiyo ni pigo na aibu kwa mawakala wa mabwanyenye waliosababisha ndege yetu kushikiliwa Canada. Mimi nauliza: Hivi 'mawakala wa mabwanyenye' waliosababisha ndege yetu ikamatwe Canada ni akina nani hasa?"alihoji Tundu Lissu 

No comments:

Post a Comment