MREMBO WEMA SEPETU AGOMÀ KUIGIZA FILAMU NA MAMA KANUMBA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 26 April 2018

MREMBO WEMA SEPETU AGOMÀ KUIGIZA FILAMU NA MAMA KANUMBA

Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi kuigiza filamu moja na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kwani Mwenyewe hakutaka mama yake ajiingize Kwenye sanaa.
Wema ameanika hayo huku akisisitiza kuwa kipindi wakati Kanumba yuko hai alimweleza Wema ambaye alikuwa mpenzi wake kuwa kamwe hataki mama yake ajiingize kwenye Bongo movie.
Wema alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambao walimuuliza endapo yupo tayari kucheza filamu na Mama Kanumba ambaye hivi sasa amegeukia sanaa hiyo:
“Hapana, siwezi kwa sababu Kanumba alikuwa hataki mama yake aigize na hata mimi alishaniambia, sasa nitavunja makubaliano yetu mimi na Kanumba”.
Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Wema alikataa tuhuma alizorushiwa na Mama Kanumba kuwa alipowenda nyumbani kwa Wema hakufunguliwa geti badala yake aliishia kuchomeshwa mahindi:
“Jamani…kwanza siku hiyo mimi sikuwepo kabisa, niliambiwa tu alikuja na kwa nini nifanye hivyo sasa“.

No comments:

Post a Comment