MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa penzi lake na msanii Richard Martin ‘Mavoko’ haliwezi kutengua swaumu yake kwani anayajua maadili ya Mwezi Mtukufu.
Akizungumza Lulu Diva alisema kuwa, japo Mavoko ni Mkristo, lakini hajaingilia funga yake kwani mara nyingi wanaonana baada ya futari tu na huwa ni kwa ajili ya maongezi ya kawaida na si vinginevyo.
“Unajua sasa hivi niko kwenye mfungo lakini siwezi nikasema nitaacha kumuona Mavoko mpaka mwezi huu uishe, itakuwa ngumu. Ninachokifanya kila ninapomaliza kufuturu namuona na uzuri anaheshimu swaumu yangu sana tu,” alisema Lulu.
No comments:
Post a Comment