KOMEDIANI wa Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ anaamini kuwa, soko la sinema za Kibongo haliwezi kubadilika kama sura za waigizaji ni zilezile za kila siku ambazo hata yeye amezichoka.
Akizungumza , Steve alisema kuwa, kama kila mtu anapotazama sinema anakutana na sura ya Kajala Masanja, Shamsa Ford, Aunt Ezekiel na wengine, watu wanachoka na mwisho wa siku ndipo linatokea anguko la sinema kama lilivyotokea.
Steve alisema kuwa, inatakiwa ufike wakati wale mastaa wakubwa waachie ngazi na kuwapa nafasi wengine ili watu waone ladha tofauti maana sura zao zimechosha mashabiki.
“Ninachokipigania ni kwamba waigizaji wakubwa wabaki na haki miliki zao, lakini sura za mastaa haohao zinachosha maana hata mimi nimezichoka,” alisema Steve.
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment