Ikiwa leo ni siku ya wapendanao (valentine day), msanii wa muziki Bongo, Tunda Man amefunguka sifa ambazo alikuwa akizihitaji kwa mwanamke.
Muimbaji huyo ambaye ameshaoa amezungumza kuwa mwanamke mweupe na mwenye nywele ndefu ni moja ya sifa zilizomvutia kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake hadi kupelekea kumuoa.
“Chakwanza nilikuwa napenda mwanamke ambaye ni mweupe, cha pili nilikuwa napenda mwanamke mwenye nywele ndefu, sipendi mwenye nywele fupi, kiufupi sipindi nywele fupi, nywele ndefu nakuwa sizichoki, unatamani kuziona kila muda,” amesema Tunda Man.
Tunda Man ametaja sifa nyingine alizokuwa akizihitaji ni pamoja na mwanamke aliyesoma ili kuweza kushauriana na kushirikiana katika mambo kadha wakadha, awe anajua dini, pia asiwe mfupi
No comments:
Post a Comment