Waziri Mwigulu Nchemba ametoa onyo kali akiwa mpakani mwa Tanzania na Uganda. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 8 October 2017

Waziri Mwigulu Nchemba ametoa onyo kali akiwa mpakani mwa Tanzania na Uganda.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka watumishi wa Umma na wananchi wa wilaya ya misenyi ambao waishio karibu na mpaka wa Mutukula kutoshirikiana na wahalifu kukamilisha mambo yao kwani kufanya hivyo ni kosa kubwa na hatua kali zitachukuliwa juu yao hasa wanaohusika na kuwaingiza wahamiaji haramu.

Hayo ameyasema akiwa ziarani mkoa wa Kagera wilaya ya misenyi katika mpaka wa Tanzania na Uganda (Mutukula) kukagua utendaji kazi wa idara ambazo zipo chini ya wizara yake na changamoto zinazoeakabili kwa ajili ya kuzitatua ili kumaliza kabisa tatizo la wahamiaji haramu nchini.

Waziri Mwigulu amewaahidi idara ya uhamiaji na polisi kuwaletea magari ambayo yatasaidia katika kufanya ukaguzi katika maeneo ya mpakani na pia atawaletea rasilimali watu kuongeza ufanyaji kazi zaidi.

Naye mkuu wa wilaya ya Misenyi Kanali Denis Filangali Mwila amesema kwasasa wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa vitendeo kazi kwa idara mambazo zipo mpakani ambapo inachangia kuingizwa kwa bidhaa kwa magendo na kupitisha wahamiaji haramu ambao wanatoka nchi za jirani.

No comments:

Post a Comment