MREMBO WEMA SEPETU AMECHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KATIKA MAENDELEO YA MWANAMUZIKI DIAMOND PLATINUM - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 14 June 2017

MREMBO WEMA SEPETU AMECHANGIA KWA KIASI KIKUBWA KATIKA MAENDELEO YA MWANAMUZIKI DIAMOND PLATINUM

Mrembo aliye kuwa miss Tanzania 2006 Wema Sepetu na pia aliye kuwa mpenzi wa zamani wa Diamond Platinum bado ana umuhimu sana kwa mwanamuziki huyu ambaye anaiwakilisha Tanzania ndani na njee ya mipaka yake.
Msanii Diamond Platinum amefunguka kuzungumzia mchango wa mrembo Wema Sepetu kwenye perfume yake ya CHIBU PERFUME na kasema yeye na Wema wanakutana na kuongea sana na wakati mwingine hushauriwa  mambo mengi ya kibiashara na mwanadada huyo ambaye alikuwa mpenzi wake.
“Mimi na Wema labda watu hawajui sisi tunaongea sana na wakati mwingine tunakutana mara kwa mara japo sio kwenye media, kila mtu kwa sasa ana mahusiano yake tofauti yeye ana familia yake na mimi nina familia yangu , hata ukiangalia kwenye perfume yangu lile neno THE SCENT YOU DESERVE alitoa wema” yalikuwa ni maneno ya Diamond Platinum kumuhusu wema.
Mwanamuziki huyu kwa sasa yupo kwenye mahusiano na Zari na tayari ameshakuwa baba wa watoto wawili, kinacho mfanya Diamond kutulia na Zari anataka familia bora kwani wakiachana yeye na Zari watoto wataishi vipi kwa hiyo atabaki na Zari kwa kusudi la kujenga msingi imara katika familia.
Kwa picha na matukio zaidi nimeleta hapa chini pia kwa story zaidi tembelea instagram page yangu @erickpicson

No comments:

Post a Comment