Shilole na Mume wake wanasaka mtoto . - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 27 February 2018

Shilole na Mume wake wanasaka mtoto .

STAA wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameeleza kuwa baada ya kuingia kwenye ndoa miezi kadhaa iliyopita kwa sasa yeye na mumewe, Ashraf Uchebe wako kwenye harakati za kusaka mtoto.

Akizungumza , Shilole alisema kama kawaida ya watu wengi huwa wanatarajia tu baada ya ndoa waone matunda ambayo ni mtoto, yeye na mumewe wako kwenye kutafuta mtoto na Mungu akimjalia atapata.

“Kuhusu suala la mtoto kwa kweli ndiyo tunatafuta na Mungu akipenda tutapata tu maana kila kitu hupangwa na yeye,” alisema Shilole.

No comments:

Post a Comment