NIYONZIMA AIFUATA SIMBA AFRICA KUSINI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 19 July 2017

NIYONZIMA AIFUATA SIMBA AFRICA KUSINI.

KIUNGO mpya wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima , aliyesajiliwa akitokea Yanga, kwa mara ya kwanza ataungana na nyota wenzake wa timu hiyo, Julai 29, mwaka huu katika kambi ya timu hiyo nchini Afrika Kusini ‘Sauz’.
Niyonzima ametua Simba baada ya kumalizana na Yanga ambapo amemaliza mkataba huku pia klabu yake hiyo ya zamani ikiweka bayana kuwa haitaendelea naye kwa msimu ujao baada ya kushindwana kwenye masuala ya maslahi.
Simba kwa sasa wamejichimbia Sauz ambako wanaendelea na kambi yao ya siku 20 wakijiandaa na msimu ujao ambapo wanatarajiwa kurejea Agosti 6, mwaka huu kwa ajili ya siku ya Simba Day ambayo itafanyika Agosti 8, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment