Aunt Ezekiel aporomosha povu zito mtandaoni(uvumilivu umemshinda) - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 8 October 2017

Aunt Ezekiel aporomosha povu zito mtandaoni(uvumilivu umemshinda)

USIONE chaelea, ujue kimeundwa! Huo ndiyo msemo uliopo akilini mwa muigizaji nyota nchini, Aunt Ezekiel, ambaye ana uhusiano na dansa, Mose Iyobo ameshusha mvua ya matusi kwa mtu anayemtongoza mwandani wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Aunt alijikuta akijivua sifa ya mwanamke mwenye roho ya Kizungu na kuachia povu zito, baada ya kushuhudia ‘vimeseji’ inbox kwenye akaunti ya Mose ya Instagram, akitongozwa na mtu ambaye anamfahamu na huenda ni shoga yake, ila hajataka kuweka wazi ni nani.

“Nw ni mtu huyu eee...Maana nimekaa nalo rohoni naona nashindwa siwezi kuvumilia kidudu mtu kuja kuharibu familia yangu tuu kirahisi kama unavyodhani ….. Koma uliza kabla hujavamia wanaume wengine hutokaa ujisamehe! Kwa uhandsom gani aliona huyu saa hizi mkajifanya kutwa kumtongoza kama sio tuu ilimradi umeshare na fulani sasa mm sio mzungu ndugu yangu ntakukanyaga hutaamini … mbona hamkumfata alivyokuwa mabonde kuinama na tulivyoanza wote mlijifanya kushangaa ...nimelileta hapa kwakuwa naona umetaka ya mtandaoni … utafute pahala upumzike lakini unajitia ujuaji basi Karibu sana dada....Na ile posti weka tuu unafuta ya nini.... utajua akili zangu... #PUSHA wa Aslay unanihusu,” aliandika Aunt Ezekiel.

No comments:

Post a Comment