Ikiwa leo Septemba 28, 2017, mwigizaji mahiri bongo, Wema Isaac Sepetu almaarufu Keki ya Taifa, anasheherekea birthday yake, mashabiki wake wameungana kwa pamoja na kumfanyia
surprise akiwa saluni kwa kumpelekea keki na shampeni wakiwa na matarumbeta.
Kitendo hicho cha kushtukiza kilimfurahisha
Wema kiasi cha kujikuta akijichanganya nao na kuanza kukata nyonga za kufa mtu.
Wema amezaliwa Septemba 28, 1987 na leo ametimiza rasmi miaka 29.
No comments:
Post a Comment