Tambwe:Ombeni Mungu tu - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 12 October 2017

Tambwe:Ombeni Mungu tu

Dar es Salaam. Mashabiki wa soka kuanzia pale Msimbazi mpaka Jangwani wanaujua mziki wa Amissi Tambwe, wamekuwa wakimsubiri kwa hamu kurudi uwanjani kuona anafanya nini msimu huu, mwenyewe kumbe amewasikia na kuwaambia neno.
Mshambuliaji huyo hajashuka uwanjani tangu msimu huu uanze kutokana na kuwa majeruhi, lakini mwenyewe amewaambia mashabiki hasa wa Yanga kuwa waiombe Mungu, kwani anaamini mabao yatarejea Jangwani.
Tambwe alisema kuwa haamini kama kukosekana kwake ndiko kumechangia timu kupata mabao machache ikifunga manne katika mechi tano, lakini bado anaamini dua zinahitajika ili timu ifanye vizuri zaidi bila ya kujali nani anacheza.
Alisema juu ya kufunga, kila mdau wa soka anaijua kazi yake ndiyo maana anazungumza, ndiyo iliyomleta nchini, hivyo atafanya kila namna akishirikiana na wenzake, kuona wanapata mabao.
"Kama ni kufunga mabao ndiyo kazi yangu na sina wasiwasi kuhusu hilo, ni jambo la kujituma, kushirikiana  na kuomba Mungu kwa sababu tunafanikiwa kwa nguvu zake," alisema Tambwe Mfungaji Bora mara mbili wa Ligi Kuu Bara.
Mrundi huyo amefunga jumla ya mabao 65 katika Ligi Kuu tangu alipotua nchini mwaka 2013, huku mabao 45 akiifungia Yanga tangu ajiunge nayo 2014.

No comments:

Post a Comment