RAPA Tyga anaonekana kuanza kufurahia maisha mapya baada ya kumuopoa rapa mwenzake, Iggy Azalea ambapo mahaba yao kwa sasa unaambiwa yamepitiliza mpaka basi!
Juzikati, Tyga aliyewahi kuwa na uhusiano na mdogo wa mwanamitindo Kim Kardashian, Kylie Jenner alionekana akiwa ameongozana na Iggy katika tamasha kubwa la wasanii la Coachella huku wameshikana mikono na pia baada ya kuingia ndani walionekana wakiwa wameshikana kimahaba.
Hadi sasa, wawili hao wameshaonekana pamoja kimahaba sehemu kibao kama vile kwenye uzinduzi wa bidhaa za urembo za mwanamuziki Rihanna ‘Rihanna’s Fenty Beauty’, Siku ya Valentine na Tamasha la Jumanji lililofanyika Melbourne, Australia.
Ikumbukwe kwamba, Iggy aliwahi kukaririwa akisema hatakuja kuingia kwenye mapenzi na rapa mwingine baada ya kutemwa na rapa French Montana, lakini kwa Tyga anaonekana kuendelea kuwazimikia marapa.
No comments:
Post a Comment