MBUNGE wa Iringa Mjini (Chadema) Msigwa ameachiwa huru jana usiku kwa dhamana baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Msigwa ameachiwa baada ya kudhaminiwa na wadhamini wawili Alex Kimbe pamoja na Mwenyekiti wa Bavicha Iringa Leonce Marto , saa nne usiku .
Msigwa alishushwa jukwaani kwa nguvu akiwa anahutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Mlandege Manispaa ya Iringa na anatuhumiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya vyombo vya usalama.
No comments:
Post a Comment