BEKI kisiki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ , amesema kuwa licha ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kufunga mabao sita hadi sasa, lakini ana kibarua kigumu mbele yake kutokana na upinzani atakaokutana nao kutoka kwa washambuliaji wa Yanga, akiwemo Amissi Tambwe.
Okwi ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufumania nyavu kwa kuwa na mabao sita hadi sasa.
Lakini Tambwe ambaye anaanza mazoezi leo Jumatatu, akiwa uwanjani kufunga huwa ni jadi yake, hatua ambayo inampa matumaini
Cannavaro kuwa mshambuliaji huyo ataweza kumfikia Okwi na kuleta ushindani.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Cannavaro amesema kuwa, mabao sita ya Okwi kwa sasa siyo kigezo cha mshambuliaji huyo kuweza kutwaa ufungaji bora msimu huu na kudai kuwa atakutana na upinzani mkali kutoka kwa washambuliaji wa Yanga akiwemo Tambwe mara baada ya kurejea.
“Ni vigumu kumhakikishia kuwa Okwi anaweza kuwa mfungaji bora katika kipindi hiki kwani tunaamini muda upo na kwa upande wetu kuna Tambwe ambaye bado hajarejea, tunaamini atafanya vizuri na kuleta ushindani kwenye mbio za ufungaji bora.
“Pia kuna wachezaji kama Chirwa (Obrey), Ngoma (Donald) na Ajibu (Ibrahimu), wanao uwezo wa kufunga vizuri na hata kuwania ufungaji bora, hivyo ligi bado na tunaamini watafanya vyema,” alisema Cannavaro.
No comments:
Post a Comment