Snura amefunguka kuhusu kuumia kimapenzi - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 18 January 2018

Snura amefunguka kuhusu kuumia kimapenzi

MSANII wa filamu Bongo, Snura Mushi amesema kuwa, japo amekuwa akionekana kulalamika kuhusu masuala ya mapenzi, ukweli ni kwamba kinachomuuma ni kutompata mwanaume stahiki kwake, lakini hajawahi kuachwa, huwa anaacha.

Snura alifunguka hayo kutokana na kuibuka minong’ono ya mara kwa mara kuwa huenda anaongoza kwa kupewa vibuti kwenye mapenzi ndomana hachoki kulalamika kuwa na stress za mahusiano, jambo ambalo amelipinga vikali.

“Nani kakudanganya huwa naachwa hiyo haijawahi kutokea, nikiona mtu haeleweki huwa najiengua mwenyewe sisubiri anipasue kichwa changu, hivyo kinachoniliza ni kutopata mtu sahihi kwangu na siyo kuachwa na wanaume,”alisema.

No comments:

Post a Comment