UKITAJA mastaa wakubwa Bongo wenye mashabiki wengi, kamwe huwezi kuacha kutaja jina la Wema Isaac Sepetu ambaye Ijumaa Wikienda limembana na kujikuta akilipuka juu ya ishu mbalimbali ambazo ni ‘hoti’.
Hivi karibuni Wema alibeba Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike kupitia Tuzo za Sinema Zetu zilizotolewa Azam TV. Kumekuwa na minon’gono juu ya mambo mengi yaliyomhusisha Wema ikiwemo kurudiana na mpenzi wake wa zamani ambaye ni mwanamuziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Habari hizo zilieleza kwamba, Wema alirudiana na Diamond baada ya jamaa huyo kuachana na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.Kufuatia mambo hayo kusemwa mno kwenye mitandao ya kijamii na kuibua sintofahamu, Ijumaa Wikienda lilimtafuta Wema ambaye aliamua kuweka wazi kila kitu ambacho wengi walikuwa wakikizungumza bila kupata majibu sahihi;
KUCHOROPOKA KWA MIMBA
Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Wema, pole na mkasa uliokupata wa kuchoropoka kwa ujauzito wako kwa mara nyingine!
Wema: Asante, lakini hiyo mimba imetoka karibia mwezi na nusu hivi umepita.
Ijumaa Wikienda: Imekuwaje sasa watu wanaizungumzia hivi sasa?
Wema: Mimi niliweka picha moja ya mwanamke mwenye tatizo kama langu la kushika mimba kisha inatoka ndipo nikaandika; ‘My Life Story’.
Hapo ndipo watu walichukulia kama nimepatwa na janga hilo kwa wakati huu, lakini ukweli ni jambo lililonipata mwezi na nusu uliopita.
Ijumaa Wikienda: Kumbe ni kweli ulikuwa na ujauzito…je, ulikuwa na muda gani?
Wema: Kama miezi miwili tu.
Ijumaa Wikienda: Najua wewe ni staa, unajuana na watu wengi sana, sasa imeshindikana kweli kupata mtalaam wa tatizo lako?
Wema: Nimeshahangaika sana, sina la kukwambia, nimefunga mara nyingi sana, nimeamka usiku wa manane na kukesha nikiomba, basi sasa hivi nimeamua kupenda tu watoto wa watu.
Ijumaa Wikienda: Au ndiyo umekata tamaa, unataka kufunga kizazi?
Wema: Nilisema hivyo na hilo nitalimiza baada ya siku ya kuzaliwa kwangu kupita.
MIMBA YA DIAMOND
Ijumaa Wikienda: Kuna minong’ono kuwa mimba ilikuwa ni ya Diamond, ukweli ni upi?
Wema: Hakuna ukweli wowote, ni ya mtu mwingine kabisa.
AMERUDIANA NA DIAMOND?
Ijumaa Wikienda: Mbona imesemekana umerudiana rasmi na Diamond?
Wema: Hakuna lolote ila ni mshkaji wangu ambaye si unajua tumezoeana sana!?
DIAMOND NYUMBANI KWAKE
Ijumaa Wikienda: Mbona kuna taarifa kuwa anakuja kwako mara kwa mara na wewe unaenda nyumbani kwa Diamond, Madale?
Wema: Nasibu hajawahi kukanyaga kwangu ila mimi ndiye niliwahi kwenda Madale mara moja tu.
Ijumaa Wikienda: Ulikwenda kufanya nini?
Wema: Alinialika, kulikuwa na swimming part (pati ya kuogelea), ndiyo siku hiyo tu.
Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo Diamond akiamua leo kwenda moja kwa moja kwa Mama Wema kutoa mahari utalipokeaje?
Wema: Yaani Diamond, hata aache kila kitu akaniambia sasa Wema nataka kukuoa sitakubali kabisa.
Wikienda: Kwa nini na wakati inasemekana ndiye mwanaume aliyeko moyoni mwako?
Wema: Ilikuwa zamani, lakini siyo sasa kwa sababu Nasibu nimekaa naye miaka miwili. Najua alivyo na hatanisumbua sana kwa sababu mimi nilimwacha CK kwa ajili yake, matokeo yake akatoka na Meninah (msanii wa Bongo Fleva) na meseji nilizibamba. Kwa hiyo hata kwenye ndoa hawezi kubadilika.
Ijumaa Wikienda: Kwa nini uliamua kumwacha CK ukaenda kwake wakati ulikuwa unapata kila kitu hadi ukapewa jina la Madam?
Wema: Mimi hakuna kitu ninachokiangalia kama furaha yangu, niliporudi kwake nilikuwa nina furaha. Nilipokwenda Hong Kong na kuachia picha, nilikuwa nina furaha kwa hiyo sijutii kitu nilichokifanya ambacho mimi kilikuwa kinanipa furaha.
Ijumaa Wikienda: Diamond alipoachana na Zari, Zari alilalamika kuwa wewe ndiye ulikuwa chanzo cha kuachana na baba watoto wake, je unalizungumziaje?
Wema: Yaani itakuwa ni vituko sana maana mimi hakuna kitu nilichofanya cha ajabu hadi achukue hatua hiyo kwa sababu kuna matukio mengi amefanya baba mtoto wake huyo ambayo ni makubwa mno yanayofanya watu waweze kutengana, lakini siyo mimi.
MOBETO NA ZARI
Ijumaa Wikienda: Basi kama ni kuoa ungependa kumshauri Diamond amuoe nani kati ya Hamisa Mobeto na Zari?
Wema: Yeye mwenyewe tu achague anayeona anayemfaa hapo maana siwezi kumchagulia.
Ijumaa Wikienda: Mbona dada wa Diamond, Esma bado anakuita wifi na hata kwenye mtandao mlikuwa mnajinadi na ikaonekana umerudisha majeshi kwa kaka yake?
Wema: Esma ni rafiki yangu sana. Kwanza kwa ajili ya Petit Man, lakini pia tulijiachia kwa sababu ya timu za mitandaoni, lakini kulikuwa hakuna chochote cha zaidi.
BIFU NA MOBETO
Ijumaa Wikienda: Kuna tetesi wewe una bifu kubwa na Hamisa Mobeto, je, ni kweli?
Wema: Sina bifu naye ila siyo rafiki yangu kabisa.
Ijumaa Wikienda: Mbona kuna kipindi mlikuwa kama mna ukaribu hivi mpaka kwenye Instagram mlikuwa mnawekana?
Wema: Ni kweli, lakini kuna maneno aliniongelea mabaya sana, tena siyo kwa kuambiwa, kwa kusikiliza sauti, sasa nikaona huo ni unafiki kwa hiyo nikaona kila mtu achukue muda wake na hata tukikutana kila mtu na hamsini zake.
YEYE NA ZARI
Ijumaa Wikienda: Unamuongeleaje Zari?
Wema: Sina shida kabisa na yule dada na ninampenda.
VIPI KUOLEWA?
Ijumaa Wikienda: Kuna kipindi ilisikika unataka kuolewa, vipi hilo?
Wema: Walijitokeza karibu wanaume watano wanaenda, kwa mama kupeleka barua kinachotokea mama ananiita, ananiuliza mimi, sikubali kwa sababu siwezi kuolewa na mtu ambaye simjui au sijakaa naye.
Ijumaa Wikienda: Mbona hutaki sasa hivi kumweka mpenzi wako wazi?
Wema: Nimekua sasa hivi, mambo ya utoto nimeweka pembeni.
Ijumaa Wikienda: Unamzungumziaje Ali Kiba alivyoamua kuoa, tena mbali na siyo nyumbani?
Wema: Ninampongeza sana kwa mwanamuziki mkubwa kama yeye kufanya jambo hilo amejijengea heshima kubwa sana, lakini ninaamini mke yupo popote ni jinsi tu Mungu alivyokupangia wapi utampata.
Ijumaa Wikienda: Mastaa wengi sasa naona wamejiingiza kwenye mambo ya ujasiriamali, vipi kwa upande wako?
Wema: Kwa vile napenda sana watoto na bado sijapata sasa hivi, ninatarajia kufungua maduka makubwa mawili kwa ajili ya nguo za watoto litakaloitwa Little Sweetheart na hapa tayari niko kwenye hatua ya mwisho kabisa ya kumalizia lipstics zangu ambazo zitakwenda kwa jina langu.
Ijumaa Wikienda: Ni nani rafiki yako wa moyoni?
Wema: Aunt, yaani anaishi kwenye moyo wangu.
Ijumaa Wikienda: Kulikuwa na madai kuwa ulihamishwa nyumba ya Ununio kwa sababu mwenye nyumba alikuwa hapendi unavyoishi na wanaume tata, unalizumziaje hilo?
Wema: Siyo kweli, mwenye nyumba alikuwa anataka kuishi mwenyewe na mpaka leo tunawasiliana vizuri tu.
Ijumaa Wikienda: Watu wengi wanajiuliza kwa nini unapenda kuongozana na wanaume tata?
Wema: Yaani hata wakiangalia nyota yangu inazungumza kabisa, sisi wenye nyota hii tunapatana na watu hao na mimi ninawapenda sana kwa sababu ni binadamu kama walivyo wengine.
MAMA KANUMBA
Ijumaa Wikienda: Vipi kuhusu ishu ya Mama Kanumba kuja kwako kisha akadai kuchomeshwa mahindi getini?
Wema: Jamani…kwanza siku hiyo mimi sikuwepo kabisa, niliambiwa tu alikuja na kwa nini nifanye hivyo sasa.
Ijumaa Wikienda: Yeye naye anaigiza, je, unaonaje ukamshirikisha kwenye filamu yako hata moja?
Wema: Hapana, siwezi kwa sababu Kanumba alikuwa hataki mama yake aigize na hata mimi alishaniambia, sasa nitavunja makubaliano yetu mimi na Kanumba.
No comments:
Post a Comment