CHEMICAL;SIJAWAHI KUPENDWA NA STEREO KWA DHATI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 7 September 2017

CHEMICAL;SIJAWAHI KUPENDWA NA STEREO KWA DHATI.

RAPA wa kike anayefanya vizuri kwenye Hip Hop Bongo, Claudia Lubao ‘Chemical’, amefunguka kuwa, msanii Stereo ambaye amekuwa akijanasibu kwenye vyombo vya habari kwamba anampenda, ukweli ni kwamba mwanamuziki huyo hajawahi kumpenda kwa dhati.

Chemical alisema kuwa, hajawahi kupendwa kwa dhati na
Stereo kwa kuwa hata siku moja, hajawahi kuelezwa kitu chochote kinachohusu mapenzi na rapa huyo, zaidi ya kumsikia tu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Siwezi kujiongopea kwamba nimewahi kupendwa na Stereo, hata mara moja rapa huyo hajawahi kunipenda, nasema hivyo kwa sababu hajawahi kunifungukia live, ninaishia kumsikia tu kwenye media na mitandao ya kijamii,” alisema Chemical.

No comments:

Post a Comment