Picha za Lissu hadharani - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 18 October 2017

Picha za Lissu hadharani

Kwa mara ya kwanza, picha ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) imeonekana hadharani baada ya kuwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) tangu Septembea 7.

Lissu ameonekana leo Jumatano kupitia picha akiwa amekaa katika kitanda cha Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Katika picha hizo, Lissu anaonekana akiwa mwenye tabasamu huku akiwa amepunga mkono kuashiria kuwasalimu ndugu, jamaa na marafiki zake.

Picha hizo zimekuwa gumzo katika mitandao mbalimbali ya kijamii na zimekuwa zikisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii.

Jana Jumanne, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe aliwaambia waandishi wa habari kuwa hali ya Lissu inaendelea vizuri na kwamba picha zake za video zingetolewa wakati wowote.

No comments:

Post a Comment