ISIS yatuma vitisho kwa Cristiano Ronaldo - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Monday, 30 October 2017

ISIS yatuma vitisho kwa Cristiano Ronaldo

London, England. Baada ya Neymar na Messi kupokea vitisho kundi la ISIS limemtumia ujumbe huo mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa, Cristiano Ronaldo

Kundi la dola la Kislamu limeendelea kutuma ujumbe wa vitisho kwa nyota wanasoka baada ya kumtumia ujumbe huo Ronaldo katika kuelekea katika fainali za Kombe la Dunia 2018, Russia.

Neymar, Lionel Messi na kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps tayari wameshapokea ujumbe wa vitisho kutoka kwa ISIS kupitia picha zilizochapishwa kwenye tovuti yao.

Katika tovuti SITE Intel Group imeonyesha picha ya Ronaldo akiwa amepiga magoti huku jicho lake moja likiwa jeusi na nyuma yake amesimama mtu mwenye kisu mkononi.

Picha hiyo ya Ronaldo chini yake iliwekwa ujumbe uliosomeka "Neno letu ni hiki unachokiona, siyo kile unachosikia," ulisomeka ujumbe huo na kuongeza. "Kwa hiyo, subiri, tunakusubiri."

No comments:

Post a Comment