Kocha yanga aipa dhamani Simba - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 29 October 2017

Kocha yanga aipa dhamani Simba

Kocha Msaidizi wa Yanga, SHADRACK Nsajigwa ameizungumzia mechi yao na Simba kwamba pande zote mbili zilionekana kuwa na hamu ya ushindi na kupelekea uwiano wa viwango.

Nsajigwa alisema kila timu ilikuwa inatawala mchezo kwa vipindi na kupelekea kuzaa sare ya bao 1-1.

Kabla ya timu hizo kukutana tayari zilikuwa na mazingira mazuri ya mechi zao za mwisho ambapo Yanga, iliwafunga Stand United mabao 4-0, huku Simba wakiwafunga Njombe Mji, mabao 4-0, jambo lililowafanya wachezaji wawe katika ari ya kujiamini.

Nsajigwa anasema, "Haikuwa mechi rahisi kama mnavyojua hizi klabu zilivyo na ushindani wa jadi, hata hivyo tunashukuru hatujapoteza, hii pointi moja ni hatua kwetu," anasema.

Huku akisisitiza kwamba akili zao wanaelekeza kwenye mechi za mbele, lengo ikiwa ni kuandika historia ya kutwaa ubingwa mara nne, mfululizo.

No comments:

Post a Comment