MWANAHERI AFUNGUKA KUHUSU KUIACHA TASNIA YA FILAMU - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 2 May 2018

MWANAHERI AFUNGUKA KUHUSU KUIACHA TASNIA YA FILAMU

LICHA ya madai kwamba amepigwa stop kuendelea kucheza filamu na mumewe, Khamis baada ya kuolewa hivi karibuni, mrembo wa filamu za Kibongo, Mwanaheri Ahmed ‘Mwana’ ameibuka na kueleza ukweli.

 Mwana  alifunguka kuwa, amekuwa akiyasikia madai hayo, lakini ukweli ni kwamba hata iweje, kamwe hawezi kuachana na kazi yake ya filamu kwani ni fani anayoipenda licha ya kuwa ana elimu kubwa, lakini aliachana na kuajiriwa na kufanya kile alichokuwa anakipenda na mumewe anaheshimu hilo.

“Mume wangu anaiheshimu na anaipenda sana kazi yangu hivyo hawezi kunizuia kuigiza, bado ninaendelea na sanaa kama kawaida maana ndoa hainizuii chochote,” alisema Mwana.

No comments:

Post a Comment