NANDY NA BILL NAS WAMEIBUKA NA JIPYA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 2 May 2018

NANDY NA BILL NAS WAMEIBUKA NA JIPYA.

Msanii Bill Nass ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake 'Tagi Ubavu ' amefunguka na kusema kuwa kuna kazi amefanya na msanii Nandy na kudai kuwa huo wimbo utatoka wakati ukifika.
Bill Nas ameweka wazi na kudai kuwa yeye na Nandy sasa wanaendelea kuishi kama marafiki na kuwa upo wimbo wamefanya pamoja.
"Kuna wimbo tumefanya pamoja, wimbo umefanywa chini ya S2KIZZY hivyo naamini muda ukifika utatoka tu ila nachojua ni wimbo mkali, kuhusu jambo ambalo limetokea kuhusu mimi na yeye tayari nilishaomba radhi kwa wananchi na sasa maisha ya kawaida yanaendelea, hivyo hatuna tofauti yoyote ile kwa kuwa yule ni rafiki yangu na nina iheshimu sana familia yake akiwa pamoja na mama yake kwa kuwa ni mtu ambaye amekuwa akijitoa sana ku-support kazi za mwanaye"alisema Bill Nas 
Mbali na hilo Bill Nas amedai kuwa katika wasanii wa kike wawili ambao wanafanya vizuri nasi Vanessa Mdee pamoja na Nandy ndiyo wasanii wanaofanya vyema kwa sasa. 

No comments:

Post a Comment