AUNTY EZEKIEL :ANACHONIPA MOSE IYOBO KWANGU NI ZAIDI YA PESA - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 2 May 2018

AUNTY EZEKIEL :ANACHONIPA MOSE IYOBO KWANGU NI ZAIDI YA PESA

  
Aunty Ezekiel: Mchango wa Moze Kwangu ni Zaidi ya Pesa
MSANII nyota wa filamu nchini, Aunty Ezekiel, amesema changamoto alizokutana nazo kwenye chumba cha kujifungulia ndio sababu ya kutunga na kuandaa filamu ya 'Mama' ambayo itazinduliwa Mei 13, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Slaam jana, Aunty Ezekiel, alisema  ameamua kuandaa filamu hiyo ili kuonyesha thamani ya mama na amepanga kuizindua kwenye Ukumbi wa Mlimani City.

Alisema lengo la filamu hiyo ni kuwafanya watu na jamii kwa ujumla kuona thamani ya mama na kuwaheshimu.

“Wakati nasubiri kujifungua nikiwa kwenye kile chumba nilipitia magumu ambayo najua mama yangu aliyapitia na baada ya hapo ndipo nikajua thamani ya mama, nilifikiria nimpatie zawadi gani, lakini nikaona ni bora nitengeneze filamu ili nionyeshe thamani ya mama,” alisema

Aidha, alisema mama mara zote amekuwa na mchango mkubwa katika jamii huku akipambana zaidi na familia ikilinganishwa na kina baba.

“Naweza nikasema mama ni muhimu kuliko baba na sisi tumekuwa haturudishi upendo kwa mama zetu kuhusiana na yale waliyotutendea, nikiwa kama msanii nimeona nije na kitu ambacho kitawarudishia thamani yao,” alisema.

Alisema katika movie hiyo ambayo ameifanyia katika Kijiji cha Kisarawe mkoani Pwani, ameshirikiana na mtoto wake (Cookie) na hakutaka kumshirikisha mumewe (Mose Iobo) kwa kuwa fani yake ni mnenguaji.

“Katika kazi zetu hatuingiliani hata siku moja hawezi kuniambia leo nikawe mnenguaji, hilo siliwezi na mimi siwezi nikamuambia aje kwenye movie kwa sababu hawezi ila kwa msaada ananipatia yaani ana msaada mkubwa sana kwangu zaidi hata ya pesa,” alisema.. 

No comments:

Post a Comment