STAA wa filamu Bongo, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ ameibuka na kueleza kuwa, licha ya tasnia ya filamu (Bongo Muvi) kwa sasa kupoteza mwelekeo, anapigana kufa au kupona na lazima atairudisha heshima iliyokuwepo awali.
Akizungumza na Za Motomoto News, Batuli alisema kuwa, filamu zilikosa mwelekeo na heshima ya tasnia hiyo kupotea kutokana na kazi mbovu walizokuwa wakitoa ndiyo maana kwa sasa amejikita katika kufanya uchunguzi wa mashabiki wanataka nini hivyo atarudi na kazi zenye maudhui mapya ambayo yatawashangaza Watanzania na zitarudisha heshima ya tasnia ya filamu.
“Filamu au tamthiliya ni biashara kama zilivyo nyingine na biashara yoyote lazima uangalie soko linataka nini kwa sababu wakati tulionao sasa ni tofauti na ule wa zamani, mashabiki wanataka kazi bora na siyo uchafu kwenye runinga zao hivyo nitarudisha heshima ya Bongo Muvi kutokana na kazi ninazokuja nazo,” alisema Batuli.
Job Opportunity At Uganda Airlines- Security Manager
-
*About US:*
Uganda Airlines is the National Carrier of the Republic of Uganda based at
Entebbe International Airport. It is headquartered in Entebbe, Waki...
No comments:
Post a Comment