Haruna Niyonzima aahidi kufunga magoli zaidi ndani ya Simba SC. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday 30 September 2017

Haruna Niyonzima aahidi kufunga magoli zaidi ndani ya Simba SC.

Kiungo wa Wekundu wa Msimbazi Haruna Niyonzima amewaomba mashabiki Simba waendelee kumuombea dua ili aweze kurudi katika ubora wake wa kuzifumania nyavu.

Niyonzima amejiunga na Simba msimu huu akitokea kwa mahasimu wao, Yanga hajafanikiwa kufunga bao tangu kuanza kwa msimu, lakini amekuwa ni mchezaji anayependwa na kukubalika kwa mashabiki wa Simba.

"Nilikuwa katika kipindi kigumu kidogo cha kuzoeana na wachezaji wenzangu, lakini nafarijika sasa nimeanza kuzoea mazingira ndani ya Simba.

"Siku zote huwa naamini mimi ni mchezaji mzuri, lakini siwezi kuwa mzuri bila ushirikiano na wenzangu, hakuna mchezaji wa aina hiyo.

"Nimekuja Simba kufanya kazi, najua mashabiki wanatamani sana kuona 'makeke' yangu uwanjani, lakini wasiwe na wasiwasi siku si nyingi mambo yatakuwa mazuri," alisema kupitia gazeti la Mwanaspoti.

Mchezaji huyo hata hivyo amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba licha ya kutofunga magoli. Emmanuel Okwi ndiye kinara wa mabao kwa Simba na Ligi Kuu Bara hadi sasa akiwa na magoli sita.

No comments:

Post a Comment