Mambo ya kuzingatia kabla kutafuta mtoto katika ndoa - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Sunday, 1 October 2017

Mambo ya kuzingatia kabla kutafuta mtoto katika ndoa

Kulitunza penzi na kulea watoto ni mambo mawili ambayo hukinzana kiasi katika ndoa.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza maswali kuwa ni wakati gani naofaa kuanza kufikiria kuwa na mtoto baada ya kufunga ndoa. Wapo ambao muda mchache baada ya kufunga ndoa mwanamke huanza kuonekana akiwa na dalili za ujauzito. Wapo wengine ambao hukaa muda mrefu baada ya ndoa kabla ya kupata mtoto.

Jambo la msingi hapa siyo muda utakaopata mtoto/ watoto baada ya ndoa, ila kinachopaswa kuangaliwa hapa ni utayari wenu.

Kabla wewe na mwenza wako hamjapanga ni muda gani sahihi wa ninyi wawili kupata mtoto, inabidi mfahamu mambo yafuatayo;

Inawezekana ukawa ndio mwisho wa penzi lenu

Ndio, Unaweza ukawa unashangaa ni kwa namna gani kupata mtoto kunasababisha penzi kufikia mwisho. Ukweli ni kwamba wapenzi/ wanandoa wengi mara baada ya kupata mtoto ule ukaribu wa kimahaba baina yao huanza kupungua. hii siyo lazima kutokea na wala haiwatokei wote, lakini mara nyingi, hasa wanawake huahamishia mahaba yao zaidi kwa mtoto.

Ni kweli kulea mtoto siyo jambo la masihara, inahitaji uvumilivu na upendo. Lakini kupata mtoto isiwe chanzo cha kuharibu ukaribu baina ya wenza.

Malezi ya watoto hutoka pande zote mbili

Kabla ya kupata mtoto, wewe na mwenza wako hakikisha kuwa mnafanya maandalizi ya kutosha na mnakubaliana namna sahihi ya kumlea mtoto wenu. Jadilianeni namna sahihi ya kumkuza, namna ya kumkanya pale atakapokosea, mbinu za kutumia ili awe na tabia njema na mengine mengi hata kabla ya kuzaliwa kwa mtoto, ili iwape urahisi katika malezi.

Watoto hawataondoa matatizo katika ndoa yenu

Wanandoa wengi hudhani kuwa kupata watoto kutasuluhisha tofauti zilizopo baina yao ama kuwaweka karibu tena. Siyo kweli kwamba unapomzalia mumeo mtoto basi atazidisha upendo kwako. Japo kwa kiasi fulani mtoto katika familia huwaunganisha wazazi, lakini itafikia kipindi kama hamjasuluhisha tofauti zenu basi jua kwamba lazima kutoelewana kutarudi pale pale.

Hivyo hakikisha kuwa mnasuluhisha ugomvi na tofauti zenu mara baada tu ya zenyewe kuibuka. usipende kukaa muda mrefu ukiwa umetofautiana na mwenzi wako, kwani kwa kufanya hivi unakaribisha mawazo potofu na hatari katika mahusiano yako na mwenza wako.

No comments:

Post a Comment