WEMA SEPETU , RIYAMA ALLY WAMEWAUMBUA WANAFIKI. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 18 April 2018

WEMA SEPETU , RIYAMA ALLY WAMEWAUMBUA WANAFIKI.

WAKATI habari zikienea mitandaoni na mitaani kwamba mastaa wawili wa filamu, Wema Isaac Sepetu na Riyama Ally wako kwenye bifu, wenyewe wameibuka na kuwaumbua washakunaku na kuwaonesha kwamba wako sawa, Risasi Mchanganyiko linakupa mkanda mzima.

Awali, habari zilienea kwamba, wawili hao hawako sawa na wana bifu na hiyo ni baada ya Wema kushinda Tuzo ya Msanii Bora wa Kike kwenye Tuzo za Sinema Zetu aliyokuwa akishindania na Riyama ambapo mwanamama huyo aliangua kilio alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha runinga akisema kwamba amedhalilishwa kushindanishwa kwenye tuzo hiyo.

Kikizungumza chanzo makini kilieleza kwamba, wawili hao kwa mara ya kwanza tangu tuzo hizo zitolewe, walikutana uso kwa uso Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar ambako kulikuwa na zoezi la kumpokea msanii mwenzao, Monalisa aliyeshinda Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike Afrika huko nchini Ghana ambapo Wema na Riyama walionekana wakiwa pamoja na kuzungumza kama kawaida.

Wasanii hao walionekana kuwaumbua washakunaku waliokuwa wakisema kwamba wana bifu kwani muda mwingi walikuwa pamoja wakipiga stori na hata alipowasili Monalisa walikwenda pamoja kumpokea kwa kumkumbatia kwa pamoja kisha walichukua tuzo zake na kupiga nazo picha wakiwa wawili tu.

“Yaani Wema na Riyama wameamua kuwaumbua waliokuwa wanasema kuwa wana bifu maana walivyokutana uwanja wa ndege walionekana wakizungumza na kupiga picha pamoja na hawakuonesha kama wana tofauti yoyote,” alieleza msanii mmoja aliyekuwa uwanjani hapo aliyeomba hifadhi ya jina.

Hivi karibuni Wema alishinda tuzo mbili kwenye Tuzo za Sinema Zetu, moja ikiwa ni ya Msanii wa Kike Mwenye Ushawishi na ya pili ni ile ya Mwigizaji Bora wa Kike ambayo ilizua mjadala mzito huku wengi wakisema hakustahili kwa kuwa Riyama anaigiza vizuri kuliko yeye.

Baada ya tuzo hizo, Riyama aliangua kilio akidai kwamba alidhalilishwa kushirikishwa katika tuzo hizo na hata kama akifa ahitaji kupewa tuzo ya heshima kama wengine wafanyiwavyo.

No comments:

Post a Comment