Simba yamtema Mnigeria chapchap - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday 1 November 2017

Simba yamtema Mnigeria chapchap

Straika wa Simba Mnigeria Mussalawal Ibrahim ambaye alikuja hapa nchini kufanya majaribio katika klabu hiyo ameshindwa na huenda siku si nyingi akarudi kwao au akatafuta timu nyingine hapa nchini.

Ibrahim alijiunga na Simba wakiwa katika maandalizi ya mechi na Yanga huko Visiwani Zanzibar lakini ameshindwa kufikia kile ambacho benchi la ufundi lilikuwa linahitaji kutoka kwake na kama angeweza kufanya hivyo basi angesajiliwa.

Meneja wa Simba, Richard Robart alisema Ibrahim ni moja ya washambuliaji wazuri lakini kocha hakulidhika na kiwango ambacho alionesha katika mazoezi ambayo alikuwa akimpatia.

Robart alisema kama angeweza kufikia kile ambacho walikuwa wanahitaji benchi la ufundi lilokuwa chini ya kocha wake, Joseph Omog basi wangempa fomu ya usajili katika dirisha dogo ambalo litafunguliwa Novemba 15.

“Anamwili mkubwa anauwezo lakini kuna vitu vya kiufundi zaidi ambavyo kocha alikuwa anahitaji kutoka kwake katika mazoezi ambayo alikuwa akimpatia hakuweza kufanya kwa kiasi ambacho mwalimu alikuwa anataka,” alisema.

No comments:

Post a Comment