ALIKIBA AMEFUNGA NDOA RASMI NA MREMBO WAKE BI AMINA MJINI MOMBASA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 19 April 2018

ALIKIBA AMEFUNGA NDOA RASMI NA MREMBO WAKE BI AMINA MJINI MOMBASA.

NI FURAHA ILIYOJE! STAA wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, amefunga ndoa na mchumba wake Amina Khalef, leo asubuhi, Aprili 19, mjini Mombasa nchini Kenya.
Hakika ni furaha, shangwe, nderemo na vifijo kwa maharusi, wanafamilia na mashabiki wa Kiba mara baada ya ndoa hiyo kufungwa katika msikiti wa Ummul Kulthum, mjini Mombasa.
Katika shughuli hiyo ya kihistoria kwa msanii huyo, Kiba ameandamana na mdogo wake, Abdul Kiba na na rafiki yake ambaye ni Gavana wa Mombasa, Hassan Joho ambaye ndiye amesimamia mipango yote ya harusi hiyo nchini humo.
Ilikuwa ni baada Koran kusomwa, na Sheikh Mohammed Kagera akakinyanyua kiganja cha Alikiba na kumuozesha kwa Amina Khalef.
“Mimi Ali Saleh nimekubali kumuoa Amina Khalef kwa mahari tuliyokubaliana na ikitokea sababu ya kuachana tuachane kwa wema,” amesema Kiba wakati akifunga ndoa yake.
Katika shughuli hiyo, Kiba alivaa joho na kilemba, alishika upanga kama desturi ya tamaduni ya zinavyomtaka na baada ya kutoka msikitini waalikwa wamekwenda nyumbani kwa ndugu wa Joho, Abu Joho, Kizingo.

No comments:

Post a Comment