Irene uwoya ametoa onyo hili unapoangalia filamu zake(Hisia nzito za mapenzi) - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday 6 October 2017

Irene uwoya ametoa onyo hili unapoangalia filamu zake(Hisia nzito za mapenzi)

STAA wa filamu Bongo, Irene Uwoya ametoa sharti kwa mashabiki wake kwamba kila wanapokuwa wanataka kutazama filamu zake hasa zile za mapenzi ni vema wakawa na rimoti karibu maana huwa anakuwa ‘deep’ katika kutekeleza ‘script’ inavyotaka, hivyo ni bora kuwa na rimoti kama kutakuwa na watotopembeni au watu wanaoheshimiana.

Akibonga  Uwoya alisema kuwa, amekuwa akijituma ipasavyo katika screen za mapenzi kwa sababu ni miongoni mwa scene anazopenda kucheza kwenye filamu, kwa hiyo rimoti ni muhimu kwa watazamaji.

“Katika sanaa nasimamia mwongozo wa script, inapojitokeza suala la scene za mapenzi huwa nakamua vibaya sana, baadhi ya watu wanakwazika kwa namna ninavyocheza, lakini ushauri kwa wale wazazi ambao ni mashabiki wangu ni vema kila wanapotazama filamu zangu wawe karibu na rimoti ili kuondoa sehemu ambazo zinawakera,” alisema Uwoya.

No comments:

Post a Comment