CHIRWA NAYE AUNGANA NA KUNDI LA WACHEZAJI MAJERUHI WA YANGA. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday 11 August 2017

CHIRWA NAYE AUNGANA NA KUNDI LA WACHEZAJI MAJERUHI WA YANGA.

Mshambulizi nyota wa Yanga, Obrey Chirwa naye ni majeruhi kutokana na maumivu ya mguu.
Chirwa raia wa Zambia, hatacheza mechi za kirafiki na mazoezi analazimika kuendelea kupata matibabu.
Imeelezwa Chirwa anaungana na kundi la kipa Beno Kakolanya na kiungo wa pembeni wa Yanga, Geofrey Mwashiuya ambao pia ni majeruhi.
Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amethibitisha lakini amesema wanaendelea vizuri.
"Mnapoanza mazoezi, au wakati mnaendelea, suala la majeruhi ni kawaida kabisa. Lakini wote wanaendelea vizuri," alisema Hafidhi.
"Matumaini yetu hivi karibuni watakuwa fiti kabisa kwa kuwa kitengo cha tiba kinaendelea kufanya kazi yake."
Yanga imekuwa ikiendelea kufanya mazoezi ya nguvu chini ya Kocha George Lwandamina ili iweze kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara pamoja na kufanya vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

No comments:

Post a Comment