Niyonzima afunguka chanzo cha kifo cha Ndikumana - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 15 November 2017

Niyonzima afunguka chanzo cha kifo cha Ndikumana

Mchezaji wa Klabu ya Simba raia wa Rwanda Haruna Niyonzima amefunguka na kusema kuwa kinachodaiwa kupelekea kifo cha Mchezaji mwenzake Hamadi Ndikumana ni maumivu ya kichwa.

Akizungumza Niyonzima amesema kuwa taarifa za awali azilipotokea kutoka Rwanda, zimesema kwamba Ndikumana alianza kupata maumivu ya kichwa jioni mara baada ya kumaliza mazoezi kwenye timu yake.

Haruna amesema kwamba "Ndikumana hakuwa mgonjwa bali kwa taarifa nilizopokea ni kwamba alianza kuumwa na kichwa baada ya kumaliza mazoezi jana jioni. Alidhani ni maumivu ya kawaida kwamba na baadae yatakwisha lakini baadae yalimzidia na kuamua kwenda hosipitali na ndipo alipofariki usiku wa kuamkia leo.

Ameongeza "Ninachofahamu mimi Ndikumana alikuwa na maradhi ya moyo lakini nikipata tarifa zaidi kutoka kwa watu walipo nyumbani nitajua zaidi nini chanzo"
Kabla ya kufikwa na umauti Katauti alikuwa kocha msaidizi wa kikosi cha Rayon Sports ya Rwanda, enzi za uhai wake aliwahi kuichezea klabu ya Stand United ya Shinyanga akitokea timu ya Cyprus.

Ndikumana amewahi kuwa Mume wa muigizaji Irene Uwoya ambapo walifunga ndoa mwaka 2009 na kujaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume (Krish) kabla ya kutengana baadaye

No comments:

Post a Comment