RAMY ASHUSHA UJUMBE MZITO KUHUSU KIFO CHA AGNESS MASOGANGE . - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday 20 April 2018

RAMY ASHUSHA UJUMBE MZITO KUHUSU KIFO CHA AGNESS MASOGANGE .

Mkono  Umekuwa  Mzitoo  Hata  Kuandika  Maumivu  Niliyonayoo  Naona  Nashindwa .
Dunia  tambara  mbovu , unadeki  salama  mchana  usiku unakua mmbovu.
Umenifunza  mengi  niliyokua  siyajui , ulisema  nishkuru  mungu  watu  wakikupenda  kwani  Adui  haumjui.
Miezi  11" tumeishi  nashkuru  ulinipeleka  kupima ( Palestina ) , Nilitokwa  na  jasho  ukanicheka  ukaniambia  huwez  nipenda  kama  nikikataa  ku
pima .
Magazeti  ya  udaku  walipotaka  SABABU  sikuweza  kuweka  tofauti  zetu  HADHARANI  kwani  bado  moyoni  niliamini  ipo  siku  Tungeweza  Kumuepusha  SHETANI .
Tulikesha  Usiku  Na  Mchana  ili  Ucheze  Filamu  Yetu  Kwa  Hisia "  Ukasema  Hii  Iwe  Kumbukumbu  Yako  Kama Niliwahii  Hata  Kwenye  Kazi  Zako  Kukusaidia.

SASA  Kwanini  Filamu  Yetu  Tulitunga  jina  liitwe  #HUKUMU ?
Ilikuwaje  Story  ya  Filamu  Mwisho  Unafariki ?
KWANI  tulikua  tunatungia  iwe kweli  Hukumu  yako ???? Mungu  ndio  HAKIMU  wa  viumbe  vyote  katika  DUNIA , Umeondoka  ghafla  sanaa ,  Na  hii  pia  ni funzo  umeniachia .
#PumzikaSalama #MileleNakuombea #RIPLOVE😢

No comments:

Post a Comment