MUBASHARA KUTOKEA SONGEA:MAJIMAJI 1-0 YANGA.(KIPINDI CHA PILI DK YA 78.) - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday 16 September 2017

MUBASHARA KUTOKEA SONGEA:MAJIMAJI 1-0 YANGA.(KIPINDI CHA PILI DK YA 78.)

Dk 78, Yanga wanapata kona ya sita, inchongwa Majimaji wanaokoa na kuwa kona tena, inachongwa tena, Humud anaokoa hapa
Dk 76, Dante anafanya kazi ya ziada hapa kumdhibiti Tegete
Dk 73, presha ya mchezo inazidi kuwa kubwa zaidi na Yanga ndiyo walioongeza mashambulizi zaidi huku Majimaji wakifanya mashambulizi ya kushitukiza
Dk 70, Yanga wanafanya shambulizi kali, Chirwa anaingia vizuri lakini krosi yake inaokolewa na SalambaDk 66, Yanga wanapata kona, inachongwa wanaokoa, inarudishwa tena lakini Salamba anaokoa vizuri
SUB Dk 66 Hassan Kessy anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul
Dk 65, mpira unaonekana kuwa na presha zaidi kwa kuwa Yanga wanataka kusawazisha na Majimaji wanalinda zaidi
Dk 62, Juma Abdul yuko chini akitibiwa baada ya kugongwa usoni na Mapunda
Dk 60, Mapunda anaingia na kuachia mkwaju mwingine lakini unapita juu ya lango la Yanga
Dk 59, Ntala anafanya kosa kwa kupangua mpira unaotua kwa Tshishimbi lakini shuti lake linapaa
Dk 58, Selembe anamtoka Juma Abdul na kuachia krosi kali lakini inatua mkononi mwa Selembe
Dk 56 sasa, mpira unaonekana umechangamka kidogo ingawa Majimaji wanaoneana kuzidi kujiamini
GOOOOOOO Dk 53, Peter Mapund anaachia mkwaju mkali sana kutoka kushoto ya uwanja baada ya kupokea pasi safi ya Kaheza na kuandika bao
Dk 50, Dante anafanya kazi ya ziada kuondosha mpira langoni mwake
Dk 46 Yanga wanaonekana wameanza kwa kazi na krosi safi ya Juma Abdul inaokolewa
Dk 45, Abdulhalim Humud anaingia kuongeza nguvu upande wa Majimaji
MAPUMZIKO
Dk 45 + 2, Salamba analala na kuokoa mpira baada ya kuwa ametokwa na Ajibu
DAKIKA TATU ZA NYONGEZA
Dk 45 Rostande analazimika kutoka langoni na kuokoa mpira
Dk 44, bado hakuna bao na hakuna mashambulizi makali sana zaidi ya yale ya rasharasha
Dk 41, Kibiga anaachia shuti safi la juujuu lakini inakuwa goalkick
Dk 40, kona safi ya Kaheza, Tumba anajitwika lakini mwamuzi anasema alishacheza faulo kumsukuma Dante
Dk 39, Tshishimbi anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Selembe na kuwa kona ya Majimaji
Dk 36, Yanga wanapata kona inachongwa, Majimaji wanaokoa. Daud anairudisha Kaheza anaokoa tena
Dk 33, krosi safi ya Juma Abdul lakini Ntala analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa
Dk 31, Ngoma anapata nafasi ya kushuti lakini anaachia shuti nyanya na kipa Ntala anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 31, Hassan Juma anaruka juu na kuondosha mpira wa adhabu wa Ajibu
Dk 27, Mwashiuya anaingia vizuri lakini Juma anaokoa na kuwa kona ya tatu ya Yanga, inachongwa wanaokoa
Dk 26, Rostande ameamka, Majimaji wanachonga kona safi hapa, Tumba anapiga kichwa na kuwa goalkick
Dk 24, kipa Rostande wa Yanga anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Mapunda uliokuwa unajaa wavuni na kuwa kona, ila Mcameroon huyo yuko chini inaonekana kaumia
Dk 22, Dante anaokoa, Majimaji wanapata kona, inaokolewa vizuri na Raphael Daud
Dk 21 sasa, mpira zaidi unachezwa katikati lakini bado hakuna timu inaweka sana mpira chini kutokana na ubovu wa uwanja
Dk 18, Mpoki anamkwapua Juma Abdul na sasa yuko chini, alikuwa akijaribu kumpita lakini bahati mbaya akamgonga mguu
Dk 16, Salamba anafanya kazi ya ziada kuondosha hatari langoni mwake wakati Chirwa akivizia, inakuwa kona. Yanga wanachonga kona safi, inaokolewa
Dk 14, Juma Abdul anachelewa kuokoa, Mrwanda anaingia lakini Tshishimbi anaokoa vizuri hapa
Dk 12, Yanga wanachonga kona safi hapa lakini Majimaji wanaokoa vizuri kabisa
Dk 10, Mwashiuya anawatoka mabeki Majimaji lakini Kennedy anaokoa na sasa yuko chini pale, kona
Dk 7, Kaheza naye anaonyesha anataka kuipasua ngome ya Yanga lakini wako makini
Dk 4, MWashiuya anajaribu kuingia tena lakini Majimaji wanaondosha
Dk 1, mechi inaanza kwa kasi na Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Majimaji, lakini Tumba Sued anaondosha

No comments:

Post a Comment