SIKUZIMIA KAMA WATU WANAVYODHANI : RAMMY GALS. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 24 April 2018

SIKUZIMIA KAMA WATU WANAVYODHANI : RAMMY GALS.

Msanii wa filamu nchini Rammy Gals amefunguka na kuweka wazi kuwa kitendo ambacho kilitokea wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa mpenzi wake Agnes Gerald si kwamba alikuwa amezimia kama ambavyo watu wanasema kwenye mitandao ya kijamii.
Rammy Gals amesema hayo akiwa jijini Mbeya baada ya kumzika Masogange na kudai kuwa alipokuwa amesimama kwa muda mrefu alianza kuona anatetemeka miguuu kwa kuishiwa nguvu hivyo aliwaomba wasanii wenzake Duma pamoja na Idris Sultan wamsaidie kuondoka katika eneo hilo.
Dumma amedai kuwa wasanii hao walipoanza kumuondoa kwenye eneo hilo ndipo walipokuja mabaunsa na kumchukua kwa kumbeba wakidhani kwamba alikuwa amezimia lakini anadai hakuwa amezia bali aliishiwa nguvu tu kwa kusimama muda mrefu.
"Nilipewa jukumu kubwa la kusimama muda mrefu sana na nilivyoona hali yangu inazidi kuwa tete natetemeka miguuni nikaomba msaada kwa Duma na Idris Sultan nikawaambia jamanii nishikeni mabega mnitoe hapa nadhani nguvu zinaniishia hivyo walipoanza kunitoa ndipo walipokuja mabaunsa na kunitengua miguu na kunibebe juu kwa juu wakidhani kwamba nimezimia, unajua mtu akivaa miwani haraka haraka huwezi kujua kama macho yako yamefumba au hayajafumba hivyo nisingeweza kukataa sababu tayari nilijikuta nipo juu kikubwa niliishiwa tu nguvu lakini nilikuwa nasikia kila kitu kilichokuwa kinaendelea" alisema Rammy Gals
Mbali na hilo Rammy Gals amesema kuwa yeye na Irene Paul ni watu ambao walikuwa na matatizo na chanzo cha ugomvi wao kilikuwa kuhusiana na Masongange huyo huyo anadai kuwa msanii huyo alishawahi kumuuliza kuwa anaishi na Masogange lakini anatambua mtu ambaye anamlipia kodi? na kusema hicho ndicho kilikuwa chanzo cha ugomvi wao hivyo anaamini amefanya hivyo kuandika ujumbe ule kwa lengo la kutaka kumuharibia siku yake.

No comments:

Post a Comment