Flora afunguka kuhusu maisha ya ndoa - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday, 2 January 2018

Flora afunguka kuhusu maisha ya ndoa

Baada ya Muimbaji wa nyimbo za Injili, Madam Flora amekuwa akimposti mume wake mpya mara kwa mara, Daudi Kusekwa. 

Hatimae muimbaji huyo amesema kuwa hajawahi kujutia kuwa mke halali wa ndoa hiyo na hasikii wa haambiwi.

Madam Flora ameiambia Bongo5 leo kuwa mapenzi ni ya watu wawili, watatu anatoka wapi? alihoji

“Mume wangu ni gentle man, anajiheshimu, ana hofu ya Mungu na ana upendo wa kweli kwangu,, to be honest nina bahati kubwa na sijutii kuwa mke wake halali wa ndoa. Namshukuru sana Mungu kwa ajili ya Daudi my husband,” amesema Madam Flora.

“When it comes kwa mume wangu sisikii siambiwi maana tulipendana wawili, watatu anatoka wapi. Mapenzi ni ya wawili so ni vyema kuziba masikio na kufanya maisha yako maana maneno ya watu hayajengi zaidi hubomoa.”

Mbali na muziki wa Injili mwanamama huyo anajishughulisha na biashara ya mavazi ya harusi, magauni, suti, viatu vya maharusi vya kisasa kwa bei rahisi. Bei zake ni kuanzia 300,000 magauni mapya.

No comments:

Post a Comment