Makamu wa Rais Zimbabwe atangazwa kuwa Rais wa mpito - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Wednesday, 15 November 2017

Makamu wa Rais Zimbabwe atangazwa kuwa Rais wa mpito

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa atangazwa kuwa Rais mpya wa chama cha ZANU -PF.

Akaunti ya chama cha Zanu PF inasemama kuwa Emmerson Mnangagwa amefanywa kuwa rais wa mpito.

Mnangawa mwenye umri wa miaka 75 alifutwa kama makamu wa rais kutokana na kile serikali ilisema kuwa kutokuwa mtiifu.

Kufutwa kwake kulionekana kama nia ya kumwezesha mke wa Rais Mugabe, Grace, kufuata nyayo za mumewe na kuwa kiongozi wa Zimbabwe.

Awali alikuwa ametoa wito kwa mumewe kumfuta makamu wa rais.

Bw. Mnangagwa ambaye ni mkuu wa zamani wa ujasusi amekuwa mtu ambaye alitarajiwa kumrithi Rais Mugabe 93.

Kufutwa kwake kulimaanisha kuwa Grace Mugabe anatarajiwa kuteuliwa kuwa makamu wa rais wakati wa mkutano maalum wa chama tawala cha Zanu-PF mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment