Yanga yaibuka kidedea simba na azam zapigwa chini - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Saturday, 14 October 2017

Yanga yaibuka kidedea simba na azam zapigwa chini

Klabu ya soka ya Yanga imeendeleza ubabe mbele ya Kagera Sugar baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu wamefanikiwa kuchukua alama tatu mbele ya wenyeji wao kupitia mabao ya Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu wakati bao pekee la Kagera limefunga na Jafari Kibaya.

Yanga sasa imesogea hadi kileleni ikifikisha alama 12 baada ya michezo sita sawa na Azam FC ambayo imelazimishwa sare ya bao 1-1 na timu ya Mwadui FC kwenye mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Mwadui Complex.

Matokeo mengine kwenye mechi za leo ni sare ya 0-0 kati ya Njombe Mji na Lipuli FC, wakati Ruvu Shooting nayo imetoka sare ya 0-0 na Singida United. Ndanda FC wametoshana nguvu na Majimaji baada ya kufungana 1-1.

No comments:

Post a Comment