MKALI wa Muziki wa Bongo Fleva, Alikibaba ‘King Kiba’ amesafiri pamoja na familia yake Jumanne hii (April 17, 2018) kuelekea mjini Mombasa nchini Kenya kwaajili ya kufunga ndoa na mpenzi wake, Aminah Rikesh itayofanyika April 26, 2018 katika ukumbi wa Diamond Jubilee wa nchini humo.
Taarifa za ndoa yake ziligubikwa na usiri mkubwa hali ambayo ilivifanya vyombo vingi vya habari nchini Tanzania na Uganda kuandika tetesi za ndoa hiyo huku vingine vikienda mbali zaidi kwa kudai ndoa hiyo ilishafungwa.
Ukweli wa ndoa hii umepobainika kwamba muimbaji huyo anafunga ndoa April 26, 2018 na siku ya jana amesafiri pamoja na familia yake kwenda Mombasa Kenya.
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, ndoa hiyo itarushwa live na kituo cha runinga cha Azam TV baada ya kukunua hali ya kurusha ndoa hiyo kwa kiasi kinachodaiwa ni zaidii ya milioni 100 za Tanzania.
No comments:
Post a Comment