SHILOLE ATOA SHARTI ZITO LA KIFO CHAKE. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Friday, 27 April 2018

SHILOLE ATOA SHARTI ZITO LA KIFO CHAKE.

MWANAMUZIKI maarufu, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ ametoa sharti zito kuwa, siku akifa hatataka mwili wake ufanyiwe mbwembwe kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar kama wanavyofanyiwa mastaa wakifariki na badala yake mambo yote yamalizike msikitini.

Akizungumza na Risasi Jumamosi ikiwa ni siku chache baada ya video queen, Agness Gerald ‘Masogange’ kufariki dunia kisha kuagwa viwanjani hapo, Shilole alisema yeye anatoa agizo kuwa, ikiwa ametokea amefariki dunia leo au kesho, kama siyo kuagwa nyumbani kwake Gongo la Mboto, basi aagwe msikitini.

“Mimi sitapenda kabisa taratibu za mazishi yangu zifanyike katika Viwanja vya Leaders, ni bora kama nyumba yangu itakuwa haijamalizika basi watu wakafanyie taratibu hizo msikitini kwa sababu mimi ni mtoto wa kiislam, siwezi kuagwa kwenye viwanja ambavyo watu wanakunywa.

No comments:

Post a Comment