Wasanii Kutoa Album imekuwa dili ,wameamua kurudi enzi•• - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Tuesday 6 March 2018

Wasanii Kutoa Album imekuwa dili ,wameamua kurudi enzi••

Mwanzoni mwa miaka ya 2,000, wasanii wengi wa Bongo Fleva walikuwa wakinufaika na kazi zao, siyo jukwaani tu, bali kwa kupitia mauzo ya albam ambapo kulikuwa na makampuni mengi yaliokuwa yakinunua albam za wasanii na kuziuza.

Miongoni mwa makampuni hayo ni GMC Wasanii Promoters, Wananchi Stores na Mamu Stores ambayo yaliwahi kusimamia Albam ya Si Uliniambia ya MB Dog, A.K.A Mimi ya Ngwair (marehemu), Fahari Yako ya Mr Ebbo (marehemu), Bahati ya Mr Nice, Mjomba ya Mrisho Mpoto, Amri Kumi za Mungu ya Dudu Baya, Safari ya Ferooz na nyinginezo.
Makala haya inawachambua baadhi ya wasanii walioanza kuonesha kuwa enzi za kutoa albam zimerudi na lilikuwa ni kosa kubwa kuuacha mfumo huo.

VEE MONEY
Alianza rasmi Januari, mwaka huu kwa kuzindua albam yake ya Money Mondays nchini Kenya akiwa amewashirikisha wakali kibao akiwemo Mohombi kutoka Sweden, Konshens kutoka Jamaica na rapa namba moja barani Afrika, Cassper Nyovest na K.O wote kutoka Afrika Kusini.
Kwa wiki ya kwanza, mapokeo ya albam yake yenye nyimbo 18 yalikuwa makubwa (Kibongobongo) ambapo alifanikiwa kuuza zaidi ya nakala 700 kwa bei ya shilingi 10,000 kwa albam.
DIAMOND
A Boy From Tandale ndilo jina la albam yake alivyoliita. Albam hiyo yenye jumla ya nyimbo 20 imewashirikisha wakali kibao ndani na nje ya nchi wakiwemo P-Square, Tiwa Savage, Omarion, Neyo, Papa Wemba, Jah Prazah, Rick Ross, Morgan Heritage na Davido.
Uzinduzi rasmi wa albam hiyo yenye ngoma kali kama Sikomi, Kidogo, Nana, Wakawaka, Niache, Hallelujah na nyinginezo unatarajia kufanyika Machi 16, mwaka huu nchini Kenya.
CHIN BEES
Anasimama miongoni mwa wakali wachanga waliofanikiwa kuingiza albam sokoni katika kipindi ambacho hakukuwa na mauzo ya albam kwa wasanii wa Bongo Fleva.
Albam ya Chin inajulikana kwa jina la Ladha ikiwa imetayarishwa na kusimamiwa na Kampuni ya Wanene Entertainment. Katika albam hiyo yenye nyimbo 11, amewashirikisha maprodyuza wakali kibao wa ndani na nje ya nchi kama Thomas Crager na Mboks.
Miongoni mwa ngoma zinazopatikana katika albam hiyo ni Leo, Nitulize, Zungusha, My Baby na Mororo.
COUNTRY BOY
Kwa sasa yupo chimbo na Prodyuza S2kizzy katika kupika albam mbili mfululizo zenye nyimbo zaidi ya 40.
Akizungumza na Showbiz, Country alitaja baadhi ya nyimbo zitakazopatikana katika albam hizo zinazotarajiwa kutoka mapema kuanzia mwezi wa nne kuwa ni Aah Wapi na Turn Up.
NANDY
Kama ilivyo kwa wakali wengine, Nandy ambaye ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva waliong’ara kwa mwaka jana, anatarajia kuachia albam mwishoni mwa mwezi huu yenye nyimbo zaidi ya 13 zikiwemo Kivuruge, Wasikudanganye na One Day. Mbali na albam hiyo, Nandy yupo pia mbioni kutoa albam moja na Aslay.
BARNABA
Licha ya kumiliki lebo yake ya High Table Sounds, Barnaba yupo mbioni kuibuka na albam yake ya kwanza itakayokuwa na ngoma zaidi ya 11 ukiwemo wimbo mmoja wa dini.
Jina la albam hiyo ni Eight Eight (8/8) ikiwa na maana ya siku yake ya kuzaliwa ambapo itakuwa na ngoma zake zote kali ikiwemo Lover Boy, Sorry, Magubegube, Tunafanana, Suna, Milele Daima, Lonely, Wanifaa na Mapenzi Jeneza.

No comments:

Post a Comment