JB : TASNIA YA FILAMU HAIJAFA.. - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday, 5 April 2018

JB : TASNIA YA FILAMU HAIJAFA..

MKONGWE wa sinema za Kibongo, Jacob Stephen ‘JB’ amesema kimsingi tasnia ya filamu Bongo haijafa kama wengi wanavyodhani.

JB alisema wavivu ndiyo wanaolalamika kwamba tasnia imekufa na hailipi jambo ambalo halina ukweli wowote.

“Mimi nasikia tu kwamba watu wanasema kuwa tasnia hailipi lakini mimi inanilipa vizuri ndiyo maana tunahitaji wasanii ambao wapo vizuri kwa mfano Gabo nilicheza naye kwenye filamu ya Danija na ikafanya vizuri, Shamsa Ford nilicheza naye kwenye Zawadi Yangu na ikafanya vizuri, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kama tukizidi kuongeza juhudi,” alisema JB.

No comments:

Post a Comment