Jacob Zuma alifika mahakama kuu ya Durban leo asubuhi kusikiliza kesi yake ambayo ina mashtaka 16, yakiwemo ya rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji wa fedha.
Wafuasi wa Zuma walijikusanya maeneo ya karibu ya mahakama hiyo huku wakiimba nyimbo za kumsifu, wakisema hawatamuacha mpaka mwisho, na wengine wakikikesha kumuombea.
Kesi hiyo dhidi ya Zuma ilishwahi kufunguliwa na kusikilizwa, kisha kufutwa mwaka 2009, lakini sasa imeanza kusikilizwa tena baada ya kuondolwa madarakani, huku Rais aliyechukua wadhifa huo Cyril Ramaphosa akiahidi kukomesha vitendo vya rushwa nchini humo.
No comments:
Post a Comment