IRENE PAUL AMWAGA SIFA HIZI KWA ZARI - Erick Picson Media

Erick Picson Media

Mkali wa Matukio na Habari za Burudani

Breaking

Thursday 5 April 2018

IRENE PAUL AMWAGA SIFA HIZI KWA ZARI

MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Irene Paul amewakata vilimi mastaa wa Bongo kwa kuwaambia kuwa hakuna staa mkubwa Bongo kama Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Irene alisema mrembo huyo wa Uganda ni mfano wa kuigwa kwani anajua kutengeneza jina lake na ni mtafutaji wa kweli.
Irene Paul.
“Ni staa mkubwa, anajua kumaintain jina lake, simuoni staa wa kumshinda yeye Bongo,” alisema Irene.
Kauli hiyo iliungwa mkono na baadhi ya mashabiki waliomsikia muigizaji huyo alipokuwa kwenye utoaji wa tuzo za wasanii wa Kibongo ambazo ziliandaliwa na kituo cha Azam TV.

No comments:

Post a Comment