Hatimaye ahadi hiyo ya Alikiba kuhusu mdogo wake imetimia kwani msanii huyo ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake ya 'Jeraha' amefunga ndoa pia na moja ya mtu wake wa karibu na kufanikiwa kuongeza idadi ya wanawake katika familia yao kama ambavyo mdogo wake wa kike Zabibu anavyosema kuwa mwanzo walikuwa wawili tu yeye na mama yake lakini ameongezeka mke wa Kiba na kudai anatarajia kuongezeka mwingine wa nne karibuni ambae ndiye mke wa Abdukiba.
Kupitia mtandao wa Instagram msanii H Baba ambaye ni mtu wa karibu na kina Alikiba ameweka wazi kuwa Abdukiba leo amefunguka ndoa na kumtakia kheri kwenye siku yake hiyo muhimu katika maisha yake.
"Hongera sana Abdukiba kwakuchukua jiko lako Allah akulindie ndoa yako, jambo la kheri uja na kheri zake karibu chama la waliompendeza Mungu kwani kuoa nijambo la kheri" alisema H Baba
Alikiba na Abdukiba wanadhaniwa kuwa huenda wanaweza kufanya sherehe ya pamoja April 29, 2018 jijini Dar es Salaaam ili kufurahi na watu wao wa karibu kufuatia zoezi la wao kufunga ndoa.
No comments:
Post a Comment