Mwili wa marehemu aliyekuwa Video queen maarufu Bongo Agnes Gerald maarufu Kama Masogange anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao Wilayani Mbozi, mkoani Mbeya ambako ndiko wazazi wake waliko.
Dada wa Agnes anayejulikana kama Emma Gerald, amesema mwili wa Agnes utaagwa jijini Dar es salaam kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni leo Jumapili kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Ambapo misa itafanyika viwanjani hapo kisha kuanza safari rasmi kuelekea Mbalizi mkoani Mbeya kwa ajili ya kuupumzisha mwili wa marehemu Agnes Gerald mahali pema peponi.
“Tutaaga leo Leaders, na kisha tutasafirisha kuelekea Mbeya kwa mazishi”, amesema Emma Gerald.
Aidha imeelezwa kuwa kutakuwa na mabasi mawili yatakayobeba wasindikizaji wa mwili huo mpaka mkoani Mbeya.
Agnes Masogange amefariki jana Aprili 20, kwenye hospitali ya Mama Ngoma baada ya kulazwa kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta kwa tatizo la pumu.
No comments:
Post a Comment